SiasaPakistan
Kabul yashutumu Pakistan kuwaondoa kwa nguvu Waafghanistan
9 Aprili 2025Matangazo
Islamabad ilitangaza mwanzoni mwa Machi kuwa Kadi 800,000 za Raia wa Afghanistan zitafutwa -- ikiwa ni awamu ya pili ya mpango wa kuwafukuza nchini ambao tayari umewatimuwa karibu Waafghanistan 800,000 wasiokuwa na vibali.
Wizara ya Taliban inayoshughulika na Wakimbizi imeandika kwenye mtandao wa X kuwa kuteswa kwa Waafghanistanna nchi jirani hakukukabiliki na hakuvumiliki. Imetoa kwa makubaliano ya pamoja ya kushughulikia kufukuzwa kwao.
Wastani wa Waafghanistan 4,000 walivuka mpaka kutoka Pakistan Jumapili na Jumatatu, kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Uhamiaji - IOM. Umoja wa Mataifa unasema karibu Waafghanistan milioni tatu wanaishi Pakistan.