KABUL : Wengi wauwawa kwenye mapigano Afghanistan
30 Oktoba 2005Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani yakishirikiana na vikosi vya Afghanistan wamesema yameuwa watuhumiwa wanamgambo 14 nchini Afghanistan.
Pia katika mapambano hayo mwanajeshi mmoja wa Marekani na mmoja wa Uingereza pamoja mwanajeshi wa Afghanistan wameuwawa.Mapambano hayo ni makali kabisa kushuhudiwa katika wiki za hivi karibuni.Wanajeshi wa kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Ulinzi kutoka Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO wamekuwa wakishambuliwa mara kadhaa huko kaskazini mwa Afghanistan lakini hii ni mara ya kwanza kabisa kufanyika kwa shambulio dhidi ya kikosi hicho cha ISAF huko Mazar-i-Sharif ambao kwa kawaida ni mji wa usalama.
Machafuko ya umwagaji damu ambayo wanamgambo wenye fungamano na kundi la Al Qaeda na Taliban wanalaumiwa kuhusika nayo yamepelekea kuuwawa kwa zaidi ya watu 1,200 mwaka huu.