KABUL: Waziri Struck ziarani nchini Afghanistan
30 Agosti 2005Waziri wa ulinzi wa Ujerumani bwana Peter Struck yupo nchini Afghanistan kuyatembelea majeshi ya nchi yake yanayolinda amani katika nchi hiyo kwa niaba ya jumuiya ya NATO.
Akizungumza na waandishi habari katika mji wa Faizabad kaskazini mashariki mwa Afghanistan bwana Struck amesema walinda amani wanakabiliwa na hatari kubwa ya kushambuliwa hasa sasa wakati ambapo matayarisho ya uchaguzi wa bunge mwezi ujao, yanafanyika.
Waziri huyo wa Ujerumani pia amesema kwamba hali ya usalama nchini Afghanistan ni ya kutisha, lakini hatahivyo amehakikisha kwamba Ujerumani haina mipango ya kuondosha majeshi yake ya kulinda amani nchini humo.
Waziri Struck pia amefahamisha kwamba nchi yake inakusudia kuongeza idadi ya askari hadi kufikia alfu tatu.
Kwa sasa Ujerumani ina askari alfu 2200 nchini Afhganistan.
.