KABUL-Watu 60 wameuawa Afghanistan kufuatia polisi kuwarushia risasi waandamanaji.
11 Mei 2005Matangazo
Watu watatu wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa leo nchini Afghanistan,baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa na hasira.
Waandamanaji hao walikuwa wanajaribu kuyachoma moto majengo kadhaa katika mji wa mashariki wa Jalalabad,baada ya kupata tuhuma kuwa wanajeshi wa Marekani wameikufuru Koran tukufu huko Ghuba ya Guantanamo,Cuba.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia,polisi walifyatua risasi kuuelekea umati wa watu waliokuwa wamejazana katikati ya mji huo,huku wa kipiga makelele ya kuishutumu Marekani na wengine wakichoma vinyago vilivyokuwa na picha ya Rais Bush.