KABUL: Wapiganaji 18 wa Taliban wauwawa
3 Agosti 2006Matangazo
Majeshi ya Aghanistan na shirika la NATO yamewaua wanamgambo 18 wa kundi la Taliban katika uvamizi wa kijiji kimoja kusini mwa Afghanistan.
Mapigano yametokea siku mbili baada ya majeshi ya NATO kuchukua uongozi wa harakati za kijeshi katika eneo la kusini kutoka kwa jeshi lililoongozwa na Marekani.
Hapo jana wapiganaji wa Taliban waliishambulia kambi ya jeshi la Danemark mkoani Helmand, na kumjeruhi mwanajeshi mmoja wa Danemark wa kikosi cha NATO.
Shambulio hilo lilikuwa la tatu dhidi ya kikosi cha Danemark tangu kilipowasili nchini Afghanstan wiki iliyopita.