KABUL: Wanamgambo wa Taliban wameuawa Afghanistan
24 Septemba 2006Matangazo
Ripoti ya wizara ya ulinzi ya Afghanistan inasema wanamgambo 40 wa Kitaliban wameuawa baada ya kupambana na vikosi vya Afghanistan na vya shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO.Mapigano hayo yalizuka siku ya Jumamosi katika wilaya ya Helmand kusini mwa nchi.Vikosi vinavyoongozwa na NATO leo hii vimesema, wanamgambo 23 waliuawa katika mapambano mawili sehemu zingine za wilaya hiyo.Kwa mujibu wa NATO zaidi ya watu 60 walioshukiwa kuwa wanamgambo, wameuawa kusini mwa Afghanistan katika kipindi cha siku chache za nyuma.