Kabul. Wanajeshi wa Ujerumani wajeruhiwa nchini Afghanistan.
26 Juni 2005Matangazo
Wanajeshi wawili wa Ujerumani na raia kadha wa Afghanistan wamejeruhiwa katika mlipuko karibu na Kunduz, kaskazini ya Afghanistan.
Msemaji wa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, amekataa kuthibitisha ripoti kuwa wanajeshi wengine wawili wa Ujerumani wameuwawa, na amesema badala yake kuwa wanajeshi hao wameorodheshwa kuwa hawajulikani waliko.
Pia amesema kuwa sababu ya mlipuko huo bado haijulikani. Kiasi cha wanajeshi 2,000 wa Bundeswehr, wamo katika jeshi linaloongozwa na NATO la kulinda amani nchini Afghanistan.
Wengi wao wako katika mji mkuu Kabul. Lakini zaidi ya wanajeshi 400 wamepelekwa katika timu za ujenzi mpya katika majimbo ya Kunduz na Faisalabad.