KABUL. Wanajeshi wa Marekani wawaua wapiganaji 12 nchini Afghanistan.
21 Aprili 2005Matangazo
Wanajeshi wa Marekani walio nchini Afghanistan wamewaua wapiganaji 12 kufuatia shambulio dhidi ya kambi yao kusini mashariki mwa nchi hiyo. Maroketi manne yalivurumishwa kwenye kambi hiyo, jambo lililowalazimu wanajeshi hao kukabiliana na wapiganaji hao. Duru za jeshi la Marekani zinasema madege ya helikopta na ndege nyengine zilitumiwa kuyajibu mashambulio hayo katika kambi ya Selerno, mkoani Khost.
Mapigano hayo yameelezewa kuwa mabaya zaidi katika miezi ya hivi punde nchini Afghanistan, ambako wanajeshi elfu 18 wa muungano wanaongozwa na jeshi la Marekani, wamekuwa wakiwasaka wanamgambo wa taliban na al Qaeda.