KABUL: Wanajeshi wa Marekani washambuliwa Afghanistan
28 Agosti 2005Matangazo
Mwanajeshi 1 wa Kimarekani ameuawa na 4 wengine wamejeruhiwa katika shambulio la bomu kusini mwa mji mkuu wa Afhganistan,Kabul.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya Kimarekani,gari la deraya la wanajeshi hao,lilishambuliwa kusini-mashariki mwa nchi,karibu na mpaka wa Pakistan.Wataliban wenye itikadi kali za kiislamu wamesema kuwa wao ndio waliofanya shambulio hilo.Mashambulio yameongezeka upya nchini Afghanistan ambako uchaguzi unatazamiwa kufanywa kati kati ya mwezi wa Septemba.Mwaka huu wanajeshi 48 wa Kimarekani wameuawa nchini Afghanistan ambako kuna kiasi ya wanajeshi 30,000 wa kimataifa-ISAF.Lengo la vikosi hivyo vya amani ni kurejesha hali ya utulivu nchini baada ya serikali ya Taliban kupinduliwa mwaka 2001.