KABUL: Wanajeshi wa Kifaransa wameuawa Afghanistan
26 Agosti 2006Matangazo
Wanajeshi 2 wa Ufaransa wameuawa katika mapigano na wanamgambo wa Kitaliban,mashariki mwa Afghanistan.Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Ufaransa mjini Paris,wanajeshi wengine 2 walijeruhiwa katika mapambano hayo.Ufaransa ina kama wanajeshi 200 katika kikosi cha madola shirika nchini Afghanistan,ambacho huongozwa na Marekani katika operesheni maalum ya kupigana dhidi ya Wataliban,hasa karibu na mpaka wa Pakistan.Wanajeshi wengine 800 wa Ufaransa ni sehemu ya vikosi vya kimataifa vinavyoongozwa na NATO kulinda usalama nchini Afghanistan.