KABUL: Waingereza 4 wajeruhiwa Afghanistan
9 Oktoba 2005Matangazo
Waingereza 4 wamejeruhiwa katika wilaya ya Kandahar,kusini mwa Afghanistan,baada ya gari lao kugongwa na gari la mwanamgambo aliekuwa na bomu.Afisa wa Kiafghanistan wa ngazi ya juu amesema,shambulio hilo limetokea katika barabara kuu iliyokuwa na magari mengi,kiasi ya kilomita 1 kutoka kituo cha kijeshi cha Kimarekani.Gavana wa Kandahar,Assadullah Khalid amesema,Waingereza hao 4 walikwenda Kandahar kwa ziara rasmi ya kuisaidia serikali ya eneo hilo kuhusu sheria za forodhani.