KABUL: Waasi 12 wameuawa nchini Afghanistan
16 Septemba 2007Matangazo
Si chini ya wanamgambo 12 wameuawa kusini mwa Afghanistan.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani nchini Afghanistan,vikosi vya Afghanistan vikishirikiana na vikosi vya kimataifa vilipambana na waasi katika Wilaya ya Helmand.Vikosi vya anga pia viliitwa kusaidia.Mapigano hayo yalizuka baada ya kama waasi 40 kuwashambulia wanajeshi waliokuwa wakipiga doria.