KABUL: Ujerumani itaendelea kuisaidia Afghanistan
21 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amekutana na rais wa Afghanistan Hamid Karzai,na amesema Ujerumani itaendelea kuisadia Afghanistan.Hii leo alipotembelea chuo cha polisi kinachoendeshwa na Ujerumani,alisema,muda wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi unaweza kurefushwa hata baada ya mwaka 2006.Kwa upande mwingine,rais Karzai amesema,Afghanistan bado inashughulika na kazi za kuijenga nchi upya na kijeshi,ingali dhaifu. Steinmeier amesema,tangu mwaka jana,hali ya usalama nchini Afghanistan imezidi kuwa mbaya.