KABUL : Uchaguzi wamalizika Afghanistan
19 Septemba 2005Matangazo
Kamishna wa uchaguzi nchini Afghanistan ametangaza kumalizika kwa rasmi kwa uchaguzi wa kwanza wa bunge nchini humo kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu.
Uchaguzi huo umefanyika huku kukiwa na ulinzi mkali ambapo zaidi ya wanajeshi wa kimataifa 30,000 na wale wa Afghanistan 100,000 wakiwa wamewekwa kulinda vituo vya kupigia kura.Zaidi ya Waafghanistan milioni 12 walijiandikisha kupiga kura na wamejitokeza kwa wingi licha ya tishio la umwagaji damu na wito wa Taliban iliyon’golewa madarakani kutaka kususiwa kwa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unakamilisha mchakato wa mpito uliokubaliwa na viongozi wa kikabila wa Afghanistan katika mkutano wa Bonn hapo mwaka 2001.