KABUL: Steinmeier amaliza ziara yake Afghanistan
23 Agosti 2006Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier akikamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Afghanistan amesema misaada inayotolewa na Ujerumani kwa Afghanistan inahitaji kushughulikiwa upya.Akaongezea kuwa atazungumza na mawaziri wenzake katika wizara za ulinzi,mambo ya ndani na misaada ya maendeleo kuhusu mada hiyo.Wakati huo huo akasisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kuviweka vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan licha ya kuongezeka kwa mashambulio ya waasi wa Kiislamu.Hapo awali waziri Steinmeier aliwatembelea wanajeshi wa Kijerumani katika vituo vyao vya Mazar-i-Sharif na Kunduz kaskazini mwa Afghanistan.