Kabul: Steinmeier ahiidi msaada Afghanistan.
22 Agosti 2006Waziri wa masuala ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir ameahidi kuendeleza misaada kwa Afghanistan kutokana na kuongezeka kwa umwagaji wa damu nchini humo.
Baada ya mazungumzo yake na rais wa Afghanistan Hamid Karzai huko Kabul, Steinmeier amesema kuwa anaimani kwamba bunge la Ujerumani katika miezi ijayo litaongeza mamlaka ya vikosi vya kijeshi vya Ujerumani vilivyoko Afghanistan.
Hata hivyo waziri huyo amefuta uwezekano wa kuongeza wanajeshi katika kikosi kilichoko huko.
Aidha Steinmeier katika maelezo yake kuhusu hali ya usalama nchini Afghanistani amesema.
„Hali ya usalama nchini Afghanistan inatulazimisha tufikirie ikiwa msaada wetu unatosha au ikiwa hali inatubidi sisi wajerumani ama Umoja wa Ulaya kwa jumla tuongeze msaada“.
Waziri Steinmeier hii leo anatarajiwa kuwatembelea wanajeshi wa Ujerumani wanaotumika kama sehemu ya kikosi cha kimataifa cha usaidizi wa usalama kaskazini mwa nchi hiyo.