KABUL: Steinemeier kutembelea vikosi vya Ujerumani
21 Agosti 2006Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier yupo Kabul nchini Afghanistan. Huko anakutana na rais Hamid Karzai na viongozi wengine.Mada kuu zinazotazamiwa kujadiliwa ni mapigano yanayozidi kuongezeka nchini humo na vile vile juhudi za kuijenga upya nchi hiyo.Steinmeier amewasili siku iliyoshuhudia mapambano makali kati ya wanamgambo wa Kitaliban na vikosi vya Afghanistan na majeshi ya Shirika la Kujihami la Magharibi NATO,kusini mwa nchi.Zaidi ya wanamgambo 70 na wanajeshi 5 wa Afghanistan waliuawa katika mapigano hayo yaliyozuka katika wilaya ya Kandahar.Siku ya jumanne waziri Steinmeier anatazamia kwenda Mazar-i-Sharif na Kunduz,kuvitembelea vikosi vya Ujerumani.Wanajeshi wa Ujerumani miezi miwili ya nyuma,walipokea uongozi ya majeshi ya amani ya kimataifa yalio chini ya uongozi wa NATO, kaskazini mwa Afghanistan.