KABUL: Shambulio la bomu Afghanistan limeuwa watu 17
28 Agosti 2006Matangazo
Hadi watu 17 wameuawa na wengine 47 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga kusini mwa Afghanistan.Maafisa nchini humo wamesema mtu aliejitolea muhanga aliripua bomu katika soko lililojaa watu,karibu na kituo cha polisi cha Lashkar Gah,mji mkuu wa wilaya ya Helmand.Mtu aliedai kuwa ni msemaji wa Taliban amedai kuwa wamehusika na shambulio hilo.