KABUL: Rumsfeld ziarani Afghanistan
11 Julai 2006Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld amewasili mji mkuu wa Afhanistan,Kabul kwa majadiliano na rais wa nchi hiyo,Hamid Karzai. Ziara hiyo inafanywa wakati ambapo majeshi ya mfungamano yakiongozwa na Marekani yameimarisha operesheni za kuwasaka wapiganaji wa Kitaliban kusini mwa Afghanistan.Zaidi ya watu 30 walioshukiwa kuwa wapiganaji wa Kitaliban wameuawa na vikosi vya Marekani na Afghanistan mapema hii leo.