Kabul. Mwanajeshi mmoja wa Marekani aokolewa nchini Afghanistan.
4 Julai 2005Matangazo
Majeshi ya Marekani nchini Afghanistan yamempata mwanajeshi mmoja wa kikosi maalum cha doria, siku tano baada ya kundi la wanajeshi hao kutoweka baada ya kushambuliwa.
Wanajeshi huyo aliyeokolowa alipatikana na wanajeshi ambao walikuwa wakihusika katika msako mkubwa tangu maafisa wa jeshi hilo kupoteza mawasiliano na kundi hilo la wanajeshi Jumanne iliyopita.
Mara baada ya kundi hilo la wanajeshi kupotea, helikopta maalum iliyotumwa kuwatafuta ilianguka karibu na eneo ambalo ilitumwa, na kuuwa wanajeshi 16 wa Marekani waliokuwamo katika helikopta hiyo.
Mwanajeshi huyo aliyeokolewa amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu.