Kabul. Miili ya polisi waliouwawa nchini afghanistan yapatikana.
11 Julai 2005Matangazo
Maafisa nchini Afghanistan wamepata miili ya polisi sita ikiwa haina vichwa ikiwa imewekwa karibu na mpaka na Pakistan. Wapiganaji wa Taliban waliwavamia polisi hao siku ya Ijumaa. Kundi hilo la Taliban limesema pia kuwa limemuua komandoo mmoja wa jeshi la Marekani katika jimbo la mashariki la Kunar, lakini hadi sasa hajapatikana.
Pia mwishoni mwa wiki hii, kiasi cha watu 18 wameuwawa katika ghasia kusini mwa Afghanistan.
Wengi wa watu hao waliokufa ni wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.
Taliban pamoja na wanamgambo wanaowaunga mkono wanajaribu kuiyumbisha nchi hiyo kabla ya uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.