Kabul. Matokeo ya uchaguzi hadi mwezi ujao.
19 Septemba 2005Matangazo
Kazi ya kuhesabu kura inatarajiwa kuanza nchini Afghanistan kufuatia uchaguzi wa kwanza nchini humo wa bunge katika muda wa zaidi ya miongo mitatu.
Uchaguzi huo umefanyika huku kukiwa na ulinzi mkali ambapo zaidi ya wanajeshi 100,000 wa Afghanistan pamoja na wale wa kimataifa wakiwekwa tayari kulinda vituo vya uchaguzi.
Wapiga kura waliojitokeza wanasemekana kuwa ni wengi , licha ya vitisho vya kutokea ghasia na wito wa wapiganaji wa Taliban wa kuwataka wapiga kura kuususia uchaguzi huo.
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameeleza kuridhishwa kwake na mafanikio ya upigaji kura huo.
Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kupatikana kuanzia mapema mwezi ujao