KABUL: Maandamano yazidi kupinga kashafa dhidi ya Koran tukufu.
13 Mei 2005Matangazo
Kumetokea maandamano zaidi nchini Afghanistan ya kupinga kitendo cha kuikashif Koran tukufu na wanajeshi wa Marekani katika jela ya Guantanamo Bay.
Watu wengine watatu wameuwawa baada ya kundi la waislamu wenye hasira lilipojaribu kuingia kati kati ya mji kutoka kusini magharibi mwa mji wa Jalalabad.
Awali watu wanne waliuwawa na wengine 70 kujeruhiwa, kwengineko maelfu ya wanafunzi nao wamefanya maandamano ya amani mjini Kabul kupinga kitendo hicho.
Mkurupuko wa maandamano ulizuka tangu juzi baada ya gazeti moja kuripoti kuwa wachunguzi waliokuwa wakifuatilia visa vya mateso katika jela ya Guantanamo Bay walizikuta baadhi ya kurasa za koran tukufu ndani ya vyoo katika jela hiyo.