KABUL Kiongozi wa mkoa wa Zabul nchini Afghanistan anyongwa kwa kufungwa kamba
16 Julai 2005Matangazo
Wapiganaji wa kundi la taliban nchini Afghanistan wamemuua kwa kumfunga kamba kiongozi mmoja katika mkoa wa Zabul, kusini mwa nchi hiyo. Malik Agha, ambaye alikuwa mfuasi wa serikali ya rais Hamid Kharzai, alitekwa nyara hapo jana.
Msemaji wa kundi la taliban amesema Agha alikuwa kachero wa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan. Wanajeshi wa Marekani waliwaua wapiganaji 24 wa kundi la taliban na wanachama wa al-Qaeda katika mapigano makali karibu na mpaka wa Afghanistan. Katika shambulio la kulipiza kisasi waasi wa taliban waliwaua maofisa saba wa polisi ya Afghanistan.
Kundi la taliban limetishia kumuua mtu yeyote anayeiunga mkono serikali ya rais Hamid Karzai inayosaidiwa na mataifa ya magharibi.