KABUL: Katiba mpya yaadhinishwa Afghanistan
5 Januari 2004Matangazo
Baraza Kuu la Afghanistan lijulikanalo kana Loya Jirga limeidhinisha katiba mpya. Zaidi ya wajumbe 500 wa baraza hilo walipiga kura kuunga mkono katiba hiyo na kuundwa kwa Jamhuri ya Kiislam ya Afghanistan itakayoongozwa na Rais mwenye madaraka makubwa ambaye nyendo zake zitakuwa zikiangazwa na bunge. Kuidhinishwa kwa katiba hiyo kunafunguwa njia ya kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza huru nchini Afghanistan katika kipindi cha miaka 25.