KABUL. Idadi ya vifo vya wapiganaji wa taliban yaongezeka.
5 Mei 2005Matangazo
Idadi ya watuhumiwa wa kundi la taliban waliouwawa na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan imeongezeka na kufikia 40.
Jeshi la Marekani limetangaza kuongezeka kwa idadi hiyo kufuatia mapigano makali hii leo yaliyosababisha umwagikaji damu mwingi tangu kung´olewa mamlakani utawala wa taliban nchini humo, mwaka wa 2001.
Askari polisi mmoja wa Afghanistan aliuwawa katika mapambano hayo na wanajeshi sita wa Marekani na askari watano wa nchi hiyo wakajeruhiwa vibaya katika machafuko hayo yaliyotokea katika mkoa wa Zabul, kusini mashariki mwa nchi hiyo.