KABUL-Bibi Condoleezza Rice awasili Afghanistan.
17 Machi 2005Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice amewasili nchini Afghanistan kwa mazungumzo yatakayojadili njia za kupambana na ugaidi pamoja na vita dhidi ya dawa za kulevya.Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Marekani anakutana na Rais Hamid karzai,pamoja na maofisa wa ngazi ya juu wa kidiplomasia wa Marekani na maofisa wa kijeshi.
Dr.Rice aliwasili mjini Kabul akitokea Pakistan akiwa katika hatua yake ya tatu ya kuyatembelea mataifa sita ya Asia ambapo pia atatembelea India,China,Korea ya Kusini na Japan.Anatarajiwa kurejea mjini Islamabad,Pakistan baadae leo kwa mazungumzo zaidi na maofisa wa Pakistan.