Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila, ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuunga mkono waasi wa M23 wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda, amekutana na viongozi wa kidini katika mji wa Goma unaodhibitiwa na waasi. Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Joel Amurani, Kabila alieleza nia yake ya kusaidia kurejesha amani mashariki mwa nchi.